Alhamisi 25 Septemba 2025 - 22:42
Mauaji ya Sabra na Shatila ni ushahidi wa kudumu wa ukatili unaofanywa na Wazayuni pamoja na ushirikiano wa baadhi ya madola katika ukanda huu na ya kimataifa

Hawza/ Harakati Umma ya Lebanon katika tamko lililotolewa kutokana na kumbukumbu ya miaka arobaini na moja ya mauwaji ya kimbari ya Sabra na Shatila, ilibainisha kuwa: mauwaji hayo yenye giza hayawezi kusahaulika kamwe.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Harakati Umma ya Lebanon katika tamko hilo lililotolewa kwa munasaba wa kumbukumbu ya miaka arobaini na moja ya mauaji ya Sabra na Shatila, ilibainisha kuwa: mauwaji hayo ya kimbari yenye giza hayawezi kufutika katika historia, huu haukuwa tu uhalifu wa mauaji ya halaiki, bali pia alama ya aibu juu ya uso wa dunia iliyonyamazishwa na iliyojeruhiwa katika mwili wa Umma ambayo haitapona kamwe.

Harakati hiyo ilisema: tarehe 16 Septemba 1982, damu za Lebanon zilichanganyika na damu za Wapalestina na roho za wasio na hatia ziliangamizwa kwenye udongo wa kambi za Sabra na Shatila, mahali ambapo adui wa Kizayuni na vikundi vya wanamgambo vya kikabila vinavyomuunga mkono walitenda mojawapo ya mauwaji ya kutisha zaidi katika historia ya karne ya hivi karibuni kwa kipindi cha siku tatu, chini ya kinga ya kimataifa na ukimya wa mataifa ya Kiarabu.

Harakati Umma ilisisitiza kwamba mauwaji haya yatasalia katika moyo wa kila mtu huru na itakuwa ushahidi wa milele wa ukatili wa wakoloni wa Kizayuni, ukatili wa vyombo vyao na ushirikiano wa baadhi ya madola ya ndaniya ukanda huu na kimataifa.

Harakati hiyo iliongeza: zaidi ya miongo minne imepita bila mahakama za Lebanon au jumuiya za kimataifa kuchukua hatua za kuwafungulia mashtaka wahusika wa uhalifu huu, hakuna uchunguzi wa kina uliyoanzishwa na wala wauaji hawajakamatwa wala kushtakiwa, badala yake jinai hii, kama uhalifu mwingine wa Wazayuni, imeachiwa na kusahaulika kisiasa.

Harakati Umma ilibainisha: wakati tunaiheshimu kumbukumbu ya jinai hii, tunashuhudia janga jipya Ghaza, ambalo ni la wazi zaidi na la kikatili zaidi, kwani watu wetu pale wako hatarini, katika mazingira ya kuzungukwa kwa vikwazo vinavyowakandamiza na baa la njaa, kwenye pazia ambalo linakumbusha vipengele vya Sabra na Shatila hasa katika suala la kiwango cha ushirikiano wa kimataifa na udhaifu ulio wazi wa mataifa ya Kiarabu.

Harakati hiyo ilibainisha kuwa: hali ya sasa huko Ghaza haina umbali mkubwa na mauaji ya siku za nyuma; ni uendelezaji wa yale yale. Ukimya kuhusu uhalifu wa leo, ni sawa na ukimya kuhusu uhalifu wa siku za nyuma, ni ushiriki katika uhalifu huo huo, bila kujali majina au nafasi zilizohusika.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha